9 Aprili 2015 - 10:12
Magaidi wa Daesh wawaachia huru mateka 200 nchini Iraq

Kundi la Daesh kwa sasa limekosa makao makuu Iraq na limeanza kukimbia maeneo mengi ya nchi hiyo, baada ya majeshi ya Iraq yakiongozwa na wataalam wa vita kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran kuwaelemea magaidi hao, ambao wanaungwa mkono na Saudia arabia.

Zaidi ya watu 200 wa kutoka jamii ya walio wachache ya Yazidi nchini Iraq wameachiwa huru na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la kigaidi la Daesh baada ya kuwa mateka kwa miezi minane. Watu hao ambao wengi wao ni wazee, waliweza kuingia salama hapo jana katika jimbo la kikurdi la Kirkuk kaskazini mwa Iran. Kundi hilo la watu wa jamii ya wayazidi waliotekwa nyara kutoka jimbo la Nineveh mwezi Novemba mwaka jana, ni kundi la pili kuachiwa na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Daesh, baada ya kundi jingine la wazee 200 kuachiwa mwezi Januari mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umesema kampeni ya wanamgambo wakundi la kigaidi la Daesh ya kulenga jamii ya Yazidi kwa kuwaua, kuwateka nyara na kuwabaka ni kitendo kinachoweza kuchukulika kuwa mauaji ya halaiki.